Rais
Barack Obama amethibitisha kifo cha mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada la
Marekani Abdul-Rahman Kassig, ambaye ameuawa kwa kukatwa kichwa na kuonyeshwa
katika video iliyorushwa na kundi la Islamic State (IS)..................
Bwana
Obama amekitaja kitendo hicho kuwa "uovu uliopitiliza" na kutoa
salaam zake za rambirambi kwa familia ya Bwana Kassig, aliyekuwa na umri wa
miaka 26, ambaye alitekwa nyara nchini Syria mwaka jana.
Video
hiyo ambayo imethibitishwa na Ikulu ya Marekani, inamwonyesha mtu aliyejificha
uso akiwa amesimama juu ya kichwa cha Bwana Kassig.
Abdul-Rahman(Peter)
Kassig akionyeshwa katika picha akigawa chakula kwa wakimbizi nchini Lebanon
Mei 2013
Pia
inaonyesha kukatwa vichwa kwa raia 18 wa Syria waliotambuliwa kama maafisa wa
jeshi na marubani.
Rais
Obama amempongeza Bwana Kassig kama mtu wa kutoa msaada kwa watu wengine na
kusema " alichukuliwa kwetu katika kitendo cha uovu wa kupitiliza
uliofanywa na kikundi cha kigaidi ambacho ulimwengu unakihusisha na
unyama".
"leo
tunatoa sala zetu na rambirambi kwa wazazi na familia ya Abdul-Rahman Kassig, ambaye
pia tulimjua kwa jina la Peter," amesema.
Kauli
ya Bwana Obama imekuja wakati akirejea Marekani kutoka Australia ambako alikuwa
akihudhuria kikao cha viongozi wa nchi za G20.
Kikundi
cha IS, ambacho kinadhibiti sehemu kubwa ya Syria na Iraq, mpaka sasa kimewaua
mateka watano kutoka nchi za magharibi.
Wengine
ni Waingereza Alan Henning na David Haines, na waandishi wa habari wa Marekani
James Foley na Steven Sotloff.
Mauaji
hayo yalitekelezwa na mtu anayeaminika kuwa Mwingereza. Ndevu za mtu huyo zinafanana
na wapiganaji walioficha nyuso zao wakiwa wamepigwa picha ya video
wakimwonyesha Bwana Kassig.
Wanamgambo
wa Shia nchini Iraq wakipiga bunduki zao wakati wa mapigano na kundi la Islamic
State katika eneo la Jurf al-Sakhar
Tofauti
na video zilizotolewa siku za nyuma na kundi la IS, video hii mpya inaonyesha
sura za wapiganaji wengi wa jihad na wanaonyesha sehemu yake kuwa ni Dabiq
katika jimbo la Aleppo nchini Syria.
Bwana
Kassig alikuwa askari wa zamani wa Marekani ambaye alitumikia jeshi la nchi
hiyo nchini Iraq.
Baadaye
alifundishwa kama mtaalam wa matibabu ya dharura na kuanzisha shirika la
kukabiliana na matukio ya dharura na msaada (Sera), likisaidia kusambaza
misaada katika makambi yaliyo katika pande zote mbili za mpaka wa Syria.
Alikuwa
akiandaa mradi kwa ajili ya shirika lake la Sera alipotekwa mwezi Oktoba 2013
wakati akisafiri kuelekea mashariki mwa Syria.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment