Ikulu
ya Marekani imesema Rais Obama atatumia muda ambao watazamaji wa televisheni
nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi kutangaza mabadiliko
makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo...............
Inatarajiwa
kuwa Rais Obama atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba kuzuia
wahamiaji wapatao milioni tano kurejeshwa makwao na badala yake wapatiwe vibali
vya kufanya kazi nchini humo.
Rais
Obama amesema hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa facebook kabla ya
hotuba yake.Tangu kuingia madaraka Obama amekuwa akipigania baadhi ya
mabadiliko ikiwemo huduma ya utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa bima ya afya
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment