Wapiganaji
wa Islamic State nchini Syria wamedai kuidungua ndege ya kivita ya muungano wa
jeshi unaoongozwa na Marekani...............
Shirika
linalochunguza maswala ya haki za kibinadamu lenye makao yake mjini
London
ambalo linaunga mkono upinzani nchini Syria limesema kuwa ndege hiyo ilianguka
karibu na mji wa kazkazini wa Raqqa unaodhibitiwa na IS.
Shirika
hilo linasema kuwa rubani, raia mwarabu aliyekuwa akiendesha ndege hiyo
ametekwa.
Baadhi
ya ripoti zinadai kuwa rubani huyo ni raia wa Jordan.Jordan ni miongoni mwa
mataifa ya kiarabu ambayo yanashiriki katika mashambulzi dhidi ya Islamic
State.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment