Rais
wa Ufaransa amewataka raia wake wasishtushwe na visa vya kushambuliwa kwa
polisi na raia katika kipindi cha siku kadhaa.
Rais
Francois Hollande ameyasema hayo baada ya mtu mmoja kuendesha gari na
kulivurumisha katika soko la Krismasi lililosheheni watu, magharibi mwa mji wa
Nantes na kujeruhi watu kumi................
Waendesha
mashtaka wamesema, shambulizi hilo linafanana na lile lililotokea katika mji wa
Dijon siku ya Jumapili ambapo dereva wa gari aliyekuwa akisema kwa sauti maneno
ya kiislamu mfululizo alipowagonga wapita kwa miguu katikati mwa mji.
Na
siku ya Jumamosi, mtu mmoja alipigwa risasi na kufariki baada ya kumchoma kisu
afisa wa polisi karibu na mji wa Tours.
Hata
hivyo, wachunguzi wamesema matukio hayo hayana uhusiano na waislamu wenye
msimamo mkali, lakini mwandishi wa BBC amesema hofu imetanda nchini Ufaransa
kuhusiana na idadi ya watu wanaojiunga na makundi ya kiislamu yenye msimamo
mkali.
Kwa
upande wake, waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve, amesema
tishio lipo nchini humo na kuwahakikishia wafaransa kwamba kila kitu kinafanywa
ili kuhakikisha usalama wa raia wake
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment