Ripoti
ya Seneti Marekani imekosoa vikali zinazotumiwa na CIA, kuwahoji washukiwa wa
uhalifu, kwamba ni za kikatili na zisizofaa..................
Ripoti
ya kamati ya bunge la Seneti nchini Marekani imekosoa vikali mbinu zinazotumiwa
na Shirika la Ujasusi la nchi hiyo za kuwahoji washukiwa wa uhalifu na kuelezea
kwamba ni za kikatili na zisizofaa.
Mwenyekiti
wa kamati ya usalama ya bunge la seneti Dianne Feinstein amesema katika baadhi
ya matukio wanavyotendewa washukiwa hao ni sawa na mateso.
''Watu
waliowekwa kizuizini walipaswa kutii mbinu zilizokuwa zikitumiwa, kuvuliwa nguo
na kuachwa watupu, walikuwa wakiwekwa katika hali ya mateso ya muda mrefu.
Walikuwa wakizuiwa kulala kwa siku kadhaa, hadi saa 180- ikiwa ni sawa na siku
saba na nusu, zaidi ya wiki bila ya kulala, kawaida wakiwa wamwesimama au
katika hali ya kuwachosha na wakati huohuo mikono yao ikiwa imefungwa pamoja
juuya vichwa. Mbonu hizo za utesaji zilianzishwa baada ya shambulio la kigaidi
la Septemba 11, mwaka 2001 nchini Marekani...''
Mbinu
hizo zinazotumiwa na shirika hilo la ujasusi zimeelezwa na wabunge hao wa
seneti kuwa zinamapungufu na kwamba CIA imekuwa ikitoa taarifa zisizo sahihi
kwa umma.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment