Wakazi wa jiji la Dar es Salaam
hutumia gharama kubwa zaidi, kulipia mahitaji yao ya muhimu kuliko wenzao
wengine wa Afrika mashariki, jijini Nairobi na Kampala,utafiti uliofanywa na
Shirika linalotathimini gharama za maisha,Numbeo umeeleza.......................
Utafiti
huu ulifanywa ukihusisha miji mikubwa 22 ukiangalia uwezo wa kununua
bidhaa,biashara za migahawani, hali kadhalika utafiti huu ulijikita kwenye
gharama za juu na urahisi wa maisha ya mijini
Kwa
mujibu wa Ripoti ya Numbeo , takwimu za gharama za watumiaji kwa wakazi wa Dar
es Salaam kwenye bidhaa na huduma mbalimbali ni asilimia 62.83 ambayo imezidi
Kampala na Nairobi zenye asilimia 54.34.
Kwa
sasa Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa Afrika Mashariki na
iko nafasi ya sita barani Afrika, hata hivyo kwa mujibu wa matazamio ya Benki
ya Standard Charterd , Tanzania inaelekea kuipiku Kenya na kuwa nchi yenye
uchumi mkubwa ifikapo mwaka 2030 iwapo pato la taifa halitabadilika
chanzo BBC.
0 maoni:
Post a Comment