Polisi
wa Ufaransa
wametoa majina na picha ya washukiwa wawili waliohusika na shambulio katika
ofisi za jarida la vibonzo nchini humo.............
Polisi
wamemtaja Said Kouachi na kaka yake Cherif wanaweza kuwa watu hatari na wenye
silaha.
Cherif
Kouachi aliwahi pia na kuhusika na kupeleka wapiganaji wenye msimamo mkali wa
kidini nchini Iraq.
Vyombo
vya Habari vya Ufaransa vimesema mtu wa tatu ambaye amegunduliwa pia kama ni
mshukiwa Hamyd Mourad mwenye umri wa miaka 18 alijisalimisha polisi baada ya
kuona jila lake katika mitandao ya kijamii.
Baadhi
ya rafiki zake walisema katika mitandao hiyo kwamba alikuwa shule wakati
shambulio hilo katika ofisi za jarida la vibonzo la Charlie Hebdo likitokea,
ambako watu 12 waliuawa.
Uchunguzi
mkali bado unaendelea kuwasaka watu hao wenye silaha.
Awali
jarida hilo lilipandisha hasira kwa waislamu baada ya kuchapisha kibonzo
walichodai kuwa ni Mtume Muhamad SAW.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment