Maafisa
wa afya katika ufalme wa Thai wamesema kuwa wavulana ambao wanaogopa kuchagua
mipira ya kondomu zinazowatosha vizuri ndio chanzo cha mlipuko wa magonjwa ya
zinaa miongoni mwa vijana...............
Katika
taarifa ilioambatana na siku ya wapendanao ya Valentine-siku ambayo maafisa wa
Thai utoa onyo kuhusu mapenzi ya ujana, wizara ya afya ya uma ilionya kuwa
magonjwa ya zinaa miongoni mwa wavulana wa miaka 10 hadi19 yameongezeka mara
tano zaidi katika kipindi cha miaka 10 iliopita.
''Ni
kwa sababu ni asilimia 43 ya vijana ndio wanaotumia mipira ya kondomu na kwamba
huchagua mipira ambayo ni mikubwa ikilinganishwa na vipimo vyao huku wakiogopa
kwamba watafanyiwa masikhara kwa kuwa wadogo''.
Wizara
hiyo imeongezea kwamba inapanga kutumia dola millioni 1.4 mwaka huu ili
kugawanya zaidi ya mipira millioni 43 kwa watu wote katika ufalme huo.
Vijana
katika ufalme huo hufunzwa kutofanya ngono badala kuambiwa watumie kinga wakati
wanapotekeleza tendo hilo.
Chanzo BBC
0 maoni:
Post a Comment