Serikali ya Siera Leone inasema kuwa
inatilia maanani ripoti maalum iliyogundua kuwa takriban dola milioni 14
zilizokuwa zitumike kupambana na ugonjwa wa ebola hazijulikani zilipo..............
Msemaji
wa serikali (Abdulai Bayraytay) aliiambia BBC kuwa yeyote ambaye atapatikana
kuhusika kwenye ufisadi huo atakabiliwa na mkono wa sheria.
Mhasibu
mkuu nchini humo ameshtumu wizara ya afya na idara inayohusika na ugonjwa wa
ebola kwa kile alichokitaja kuwa ukiukaji wa sheria.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment