Treni mbili zimekosea njia huko nchini
India na kutumbukia katika mto nchini India
Treni
hizo za abiria zilitumbukia katika mto uliokuwa umefurika kufuatia mvua kubwa
katika Jimbo la Madhya Pradesh................
Shirika
la habari la Associated Press limemnunukuu mmoja wa waokoaji akisema kuwa
wamehesabu maiti 20.
zaidi
ya abiria 250 wameokolewa, baada ya mabehewa sita kutumbukia mtoni
Wakuu
wa shirika la Reli la India wanasema ajali hiyo ilitokea usiku wa manane
kuamkia jumatano.
Anil
Saksena, ni msemaji Shirika la Reli la India, amesema Treni moja ilitoka katika
njia yake huku nyingine ikifuatia nyuma yake katika njia ya kupishana, Treni
zilipoteza mwelekeo kutokana na mafuriko.
0 maoni:
Post a Comment