Kundi la wapiganaji wa
Taliban nchini Afghanistan limemteua kiongozi mpya baada ya kuuawa kwa Mullah
Mansour.
Bw Mawlawi Haibatullah
Akhundzada ndiye kiongozi mpya.
Manaibu wake watakuwa
Sirajuddin Haqqani, ambaye mtandao wake umedaiwa kutekeleza mashambulio mengi
ya mabomu Kabul, na
Mohammad Yaqoob, mwanawe mwanzilishi wa Taliban, Mullah
Omar.
Mansour aliuawa katika
mkoa wa Balochistan nchini Pakistan kwenye
shambulio lililotekelezwa na ndege
za Marekani zisizokuwa na rubani.
Rais wa Marekani Barack
Obama Jumatatu alithibitisha kifo cha Mansour Jumatatu.
KUTOKA BBC SWAHILI
0 maoni:
Post a Comment