Kundi la wapiganaji wa
Kiislamu Islamic State linakabiliana na vikosi aina mbili tofauti vinavyojaribu
kuliondoa kundi hilo katika maeneo yanahodhi nchini Syria na Iraq.Kundi la
kikurdi la muungano wa makundi yaliyojihami kaskazini mashariki mwa syria
limetangaza kuanza kwa kampeni karibu na himaya yake iliyopo katika mji wa
Raqqa.
Muungano huo unakisiwa
kupeleka wapiganaji elfu thelathini.Washington na Moscow zimethibitisha kuunga
mkono.
Nchini Iraq, vikosi
mbalimbali vya jeshi, na watu wa makabila ambayo yanaunga mkono serikali
iliyopo madarakani wanaendelea kupambana na kundi la IS katika mji wa Falluja.
0 maoni:
Post a Comment