Rais Putin amesisitiza kuwa ushindi
dhidi ya makundi yanayopigana na wanajeshi wa Rais Assad utasaidia kuanzisha
mashauriano ya amani kati ya Serikali na wapinzani aliowataja kama wazalendo.
Alisema Urusi na mataifa ya magharibi yanapaswa
kujiona kama washiriki dhidi ya adui wa pamoja - lakini wakati huohuo alilaumu
Serikali za Mataifa ya Magharibi kwa kuwa manafiki katika wajibu wao nchini
Syria. Alisema mataifa hayo yanawashambulia magaidi wengine lakini wakati
huohuo kuwatumia magaidi wengine kwa manufaa yao.
0 maoni:
Post a Comment