Mamlaka ya safari za
ndege nchini Urusi imepiga marufuku ndege za shirika la taifa la ndege la Misri
kuhudumu Urusi, msemaji wa uwanja wa ndege Moscow amesema.
Safari za ndege kutoka
Urusi hadi Misri tayari zilikuwa zimesimamishwa baada ya ndege ya Urusi
kuanguka eneo la Sinai mwezi jana.
Abiria wote 224
walifariki, wengi wao wakiwa raia wa Urusi.
Shirika hilo la Egypt
Air ndilo pekee lililokuwa limesalia likifanya safari kati ya mataifa hayo
mawili.
Vyombo ya habari Urusi
zinasema shirika hilo limepigwa marufuku kuhakikisha linatimiza matakwa ya
kiusalama.
Kundi la Sinai
Province, lenye ushirika na Islamic State, limedai kuhusika katika kuangusha
ndege ya Metrojet nambari 9268, iliyokuwa ikitoka Sharm el-Sheikh kuelekea St
Petersburg Urusi.
Mataifa ya Magharibi
yamesema kuna uwezekano mkubwa bomu lililipuka ndani ya ndege hiyo ikiwa
angani, lakini Urusi na Misri zimesema ni mapema mno kuthibitisha hayo.
Baada ya ajali hiyo,
mataifa kadha, ikiwemo Uingereza, yalisitisha safari za ndege za kuingia na
kutoka Sharm el-Sheikh, yakitaja wasiwasi kuhusu usalama.
kutoka BBC Swahili,
0 maoni:
Post a Comment