Umoja wa Mataifa
umesema serikali ya Syria imekubali kuruhusu misaada ya kibinadamu kwenda
katika mji ulizingirwa wa Madaya ambayo kuna taarifa watu wamekuwa wakifa kwa
njaa.
Shirika la Chakula la
Umoja wa Mataifa limeiambia BBC kuwa msafara wa umeingia katika mji ulikuwa
ukikaliwa na waasi katibu na mpaka na Lebanon.
Madaya ulilkuwa
umezingirwa na majeshi ya serikali na wafuasi wao wa Hezbollah kwa miezi kadhaa
picha za video katika eneo hilo zinaonyesha watu wakiwa katika hali mbaya.
Inaelezwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakilazimika kula majani na udogo badaa ya
chakula kumalizika.
Mkuu wa shirika la
chakala duniani katika ofisi za London Grey Barrow amesema maandalizi
yanafanyika kuhakikisha misaada inawafikia wanaohitaji.
"Kumekuwa na
mipango inayofanyika kabla ya magari kuingia eneo hilo labda inaweza kuwa ndani
ya saa sabini na mbili labda hilo ndilo linaweza kuwezekana. Ninaamami hadi
jumatatu tutapeleka magarai eneo hilo magari ambayo yapo tayari lakini
yanahitaji mipango."
Hata hivyo Grey
ametahadharisha eneo wanalopeleka misaada ni eneo la hatari.
"Nadhani ni lazima
tukubali tunakoenda hali ni mbaya. Tunakwenda eneo la mstari wa mbele tunapaswa
kujua tunapoingia pale hakuna hatari ya kudhurika, kwamba tutapeleka chakula
huko na mahitaji mengine tutakayobeba kwa niaba ya mashirika mengine ya
kibinadamu na tunadhani tutawafikia wale wenye mahitaji makubwa."
Kutoka BBCSwahili
0 maoni:
Post a Comment