MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

SHISHA NI MARUFUKU KUTUMIWA

Dubai imepiga marufuku wanawake waja wazito kuvuta ama hata kuingia katika migahawa inayouza Shisha .
Hatua hiyo inafuatia shinikizo la kuimarisha afya ya umma na haswa afya ya mama waja wazito.
Sheria hiyo inawadia baada ya kampeini ya kuwazuia wanawake wajawazito kuingia pahala panapovutiwa sigara jarida la aGulf News linasema.
Kampeini hiyo inayoendeshwa kwa kutumia mabango na picha ya mwanamke mjamzito akiambiwa na mwanaye aliyeko tumboni kuwa ''Uamuzi wa kuvata au la ni wako,,,sio wangu''
Mabango hayo yanaeleza kuwa watoto ambao hawajahitimu miaka 18 na wanawake wajawazito hawaruhusiwi kuvuta shisha au sigara. 
"Kauli hiyo ni ya serikali wala sio hoja ya kujadiliwa na yeyote '' alisema mkurugenzi wa afya ya umma wa Dubai bwana Marwan Al Mohammed.
Wamiliki wa vilabu vya burudani vinavyouza shisha wamekuwa wakilalamikia kutokuwepo kwa sheria zinazoharamisha wanawake wajawazito kutoingia katika vilabu hivyo.
''Sasa sheria hii inaweka bayana anayeruhusiwa kisheria kuvuta ima ana pesa au la '' aliongezea kusema.
Mwaka wa 2014 milki hiyo ya kiarabu ilipitisha sheria kali dhidi ya uvutaji wa sigara ambayo ilipiga marufuku matangazo ya aina yeyote ya kibiashara ya Sigara.
 Vilevile sheria hiyo ilipiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya gari iwapo mna mtoto mwenye chini ya umri wa miaka 12.
Aidha sasa kuna sheria inayotoa mwelekeo ya ni wapi shisha itauzwa na itaruhusiwa kuwepo umbali gani kutoka kwenye makazi ya watu.

.Kutoka BBC
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment