Alikuwa ametoa tamko lake katika hafla
iliyopeperushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha MSNBC.
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali.
Lakini muda muda mfupi baadaye,
alibadili msimamo wake na kusema ni wahudumu wa afya wanaosaidia wanawake kutoa
mimba pekee wanaofaa kuadhibiwa.
Lakini hata baada ya kusema hivyo,
alijitetea na kuongeza kuwa: “Msimamo wangu haujabadilika.”
Mgombea huyo anayeongoza katika chama
cha Republican anaunga mkono kupigwa marufuku kwa utoaji mimba, lakini kwa
kutegemea hali.
Utoaji mimba umekuwa halali nchini
Marekani tangu 1973 kufuatia uamuzi wa kihistoria wa Mahakama ya Juu nchini
humo.
KUTOKA BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment