Watu zaidi
ya 45 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu visiwani
Zanzibar katika kipindi cha miezi miwili, shirika la habari la AP limeripoti.
Shirika
hilo la habari limemnukuu afisa wa afya visiwani humo anayesema vifo hivyo
vimetokea mwezi Machin a Aprili.
Muhammed
Dahoma, ambaye ni mkurugenzi wa anayeangazia kuzuia maradhi katika wizara ya
afya, anasema watu karibu 3,000 wamelazwa hospitalini baada ya kuugua.
Ameongeza
kuwa serikali ya Zanzibar imechukua hatua kukabiliana na mlipuko huo.
Miongoni
mwa hatua zilizochukuliwa ni kupiga marufuku uuzaji wa chakula na juisi maeneo
ya wazi.
Taarifa
kutoka visiwani humo zinasema serikali pia imeamuru kufungwa kwa shule zote kwa
muda usiojulikana.
Waziri wa
elimu Riziki Pembe Juma, amenukuliwa na shirika la habari la Uchina la Xinhua,
akisema uamuzi huo umetolewa baada ya kubainika kwamba wanafunzi ni miongoni
mwa watu walioathiriwa zaidi na ugonjwa huo.
0 maoni:
Post a Comment