Yamkini bi Bule aliumwa na nyoka yapata
dakika 45 zilizotangulia katika ''shoo yake'' iliyokuwa magharibi mwa Java
Indonesia.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa
muimbaji huyo nyota alimkanyaga kimakosa nyoka huyo ambaye alikuwa sehemu ya
''shoo'' yake na kwa bahati mbaya nyoka huyo akamuuma kwenye paja.
Japo nyoka huyo alikuwa ameng'olewa
chonge zake , kwa njia moja au nyingine aliweza kum'gata na kuingiza sumu ndani
ya damu yake.
Duru zinasema kuwa alipewa dawa ya
kutuliza makali ya sumu lakini akakataa akidhania kuwa nyoka yule hakumdhuru.
Aliendelea na onyesho hilo akiwatumbuiza
mashabiki wake hadi pale alipoanza kutapika jukwani ndipo washirika wake
wakang'amua hali haikuwa nzuri.
Mara akaanza kutetemeka na kuzirai.
Walipomkimbiza hospitalini daktari
aliwaambia kuwa alikuwa ameshakata roho yake.
kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment