Lakini tayari kuna utata kwani baadhi ya
vyama vya upinzani vinasusia uchaguzi huo, ishara ya jinsi upinzani
umegawanyika hivyo kujipata katika hali hiyo hafifu mbele ya chama tawala cha
rais aliyeko madarakani, Ismael Omar Guelleh.
Upinzani umekuwa ukilalamika kwamba
serikali, haijaweka mazingira sawa ya ushindani.
Wagombea vinara wa upinzani ni Omar Elmi
Kaireh na Mohamed Daoud Chehem, lakini kwa sababu ya kutokuwa na umoja miongoni
mwao, watakuwa na kibarua kigumu na wachambuzi wa kisiasa wanasema hawatarajiwi
kuung'oa utawala wa rais Ismael Omar Guelleh ambaye amekuwa madarakani tangu
1999.
Rais Guelleh ni rais wa pili tu tangu
nchi hiyo ijikomboe kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Ufaransa mwaka wa 1977.
Djibouti ni nchi iliyozungukwa na
mataifa majirani ya Somalia, Yemen na Eritrea ambayo yamekumbwa na mizozo ya
kisiasa.
Kutoka BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment