Kampuni ya magari ya Volkswagen imetangaza kuyanunua magari ya
kampuni yake kutoka kwa wateja nchini Marekani yapatayo nusu milioni kama
sehemu ya kutimiza makubaliano yaliyofikiwa na idara ya sheria ya Marekani
dhidi ya makampuni ya kutengeneza na kashfa ya uchafuzi wa hali ya hewa.
Jaji kutoka San Francisco hajabainisha wazi kiasi ambacho
wamiliki wa magari hayo watalipwa na kampuni ya Volkswagen pale watakapo iuzia
kampuni hiyo magari yake wanayoyamiliki.
Makubaliano mengine yaliyofikiwa ni kwamba Volkswagen itatakiwa
kutoa fungu la fedha ili kuhamasisha tekinolojia ya kijani.
Wakili anayeiwakilisha kampuni ya Volkswagen Robert
Giuffra,amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya jitihada zote kuhakikisha
inapunguza uchafuzi wa hewa
Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili David Boies umesema
unataraji haki itatendeka kwa wamiliki wa magari hayo.Joyce Ertel Hulbert,ni
mmoja wa wamiliki wa magari aina ya Volkswagen yeye anadai anadai kampuni hiyo
imemuangusha
Katika hatua nyingine maafisa kutoka taasisi ya kuzuia
udanganyifu wa kifedha kutoka ufaransa,wamezivamia ofisi za Peugeot citroen
,ikiwa ni muendelezo wa uchunguza dhidi ya uchafuzi wa hewa kutokana na magari.
Msemaji wa kampuni hiyo anasema wameonyesha ushirikiano wa
kutosha katika kuchunguzwa kwao .
kutoka BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment