Mtoto
wa askofu mstaafu wa kanisa la kianglikana nchini Afrika Kusini, Desmond Tutu
amefutwa kazi yake ya ukasisi wa kanisani baada ya kufunga ndoa na mwanamke
mwenzake.
Mpho Tutu aliyekuwa
akihudumia kwenye kanisa la Anglikana alifunga ndoa hiyo mwezi uliopita na Prof
Marceline van Furth huku sheria za nchi hiyo zikiruhusu ndoa hiyo ya jinsia
moja kutokana na sheria iliyopitishwa Novemba 30, 2006. Lakini kanisa hilo la
Anglikana la Afrika Kusini bado limeendelea kupinga ndoa hizo za jinsia moja.
Aidha baada ya kitendo
hicho alichokifanya Mpho Tutu kanisa la Anglikana la Afrika Kusini limeamua
kumvua madaraka yote aliyokuwa nayo kwenye kanisa hilo kama kuongoza ibada
ibada takatifu za kanisa hilo pamoja na shughuli zote za kikanisa.
Hata hivyo Bi Tutu
amekiri kuwa sheria za kanisa hilo la kianglikana nchini Afrika kusini
zinaeleza wazi kuwa ndoa iliyoruhusiwa ni kati ya mwanamke na mwanaume pekee.
Baada ya kufunga ndoa hiyo askofu wa kanisa la Saldanha Bay alishauriwa kufuta
leseni yake, lakini Bi Tutu aliamua kuirejesha yeye mwenyewe kabla ya
kunyang’anywa.
FROM. BONGO5
0 maoni:
Post a Comment