Fujo zimezuka
katika mji mkuu wa Gabon, Libreville baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa
mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi.
Serikali imesema inawaandama "wahalifu wenye silaha" ambao awali walikuwa wameteketeza majengo ya bunge.
Bw Ping amepinga matokeo ya urais ambayo yalionyesha Rais Bongo alishinda uchaguzi kwa kura chache. Hii inampa fursa ya kuongoza taifa hilo kwa muhula mwingine wa miaka saba.
"Walishambulia mwendo wa saa 01:00 (00:00 GMT). Ni kikosi cha wanajeshi walinzi wa rais. Walikuwa wanarusha mabomu kutoka kwa helikopta na kisha baadaye wakashambulia kutoka ardhini," Bw Ping, ambaye hakuwa katika makao makuu hayo wakati huo, alisema awali.
Ameomba usaidizi kutoka kwa jamii ya kimataifa kulinda raia.
0 maoni:
Post a Comment