MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Waziri aliyesinzia mkutanoni auawa Korea Kaskazini

Rais Kim Jong-un na mkewe Ri Sol-juImage copyrightEPA
Image captionRais Kim Jong-un na mkewe Ri Sol-ju
Serikali ya Korea Kusini imesema waziri wa elimu nchini Korea Kaskazini ameuawa na maafisa wa serikali.
Tangazo la kifo cha Kim Yong-jin limetolewa na wizara ya muungano ya Seoul na limetolewa siku chache baada ya taarifa za gazeti moja kusema maafisa wawili wakuu wa Korea Kaskazini waliuawa kwa kulipuliwa kwa makombora ya kutungua ndege.
Gazeti hilo lilisema wawili hao waliuawa mapema mwezi huu.
Waziri huyo wa elimu anadaiwa kuchunguzwa kwa madai ya kuhusika katika ufisadi baada yake kusinzia katika mkutano wa kiongozi wan chi hiyo Kim Jong-un.
Kim Jong-unImage copyrightAP
Image captionWaziri huyo alichunguzwa baada ya kusinzia mkutano wa Rais Kim Jong-un
Mapema mwezi huu, naobu balozi wa Korea Kaskazini nchini Uingereza aliikimbia nchi yake na kuhamia rasmi Kusini.

kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment