Simu ya kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7, ambayo ilikuwa imethibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, imeshika moto kwenye ndege nchini Marekani.
Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa na abiria aliyekuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines.
Shirika hilo limesema abiria waliokuwa kwenye ndege moja yake, iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland, waliondolewa kwenye ndege kwa dharura kabla ya ndege hiyo kupaa Jumatano.
Kampuni ya Samsung iliwashauri watu waliokuwa wamenunua simu za Note 7 kuzirejesha kwa kampuni hiyo baada ya kugunduliwa zilikuwa na tatizo kwenye betri zake.
Samsung imesema bado inachunguza kisa hicho cha Jumatano.
kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment