MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Arsenal yapambana kiume nyumbani kwa Bournemouth

Olivier Giroud alikuwa mchezaji bora wa mtanange huo
Image captionOlivier Giroud alikuwa mchezaji bora wa mtanange huo
Arsenal imeambulia alama moja nyumbani kwa Bournemouth baada ya kutoka nyuma kwa magoli 3-0.
Ilikuwa nii kama kutimiza lengo kwa the Gunners baada ya kufunga magoli matatu ndani ya dakika 20, kabla ya hapo Bournemouth ambao walikuwa wenyeji walikuwa wakiongoza kwa magoli 3-0.
Alexis Sanches alianza kuiandikia bao la kwanza Arsenal dakika ya 70 kabla ya Lucas Perez kuandika bao la pili dakika tano baadae.
Bournemouth ilianza kuyumba baada ya nahodha wake Simon Francis kulimwa kadi nyekundu
Image captionBournemouth ilianza kuyumba baada ya nahodha wake Simon Francis kulimwa kadi nyekundu
Bournemouth ilianza kuyumba baada ya nahodha wake Simon Francis kulimwa kadi nyekundu dakika ya 83 na kuachia mwaya kwa Arsenal kuutawala zaidi mchezo ambapo dakika ya 90 Olivier Giroud aliisawazishia timu yake na kupelekea kugawana alama moja moja.
Kwa matokeo hayo Arsenal wanasalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama 42 huku AFC Bournemouth wakipanda mpaka nafasi ya tisa wakiwa na alama 25 kibindoni.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment