Ripoti kutoka Yemen, zinaeleza kuwa shambulio, lililofanywa na makamando wa Marekani, limeuwa watu kama 30, wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa al-Qaeda na raia.
Hata hivyo jeshi la Marekani linasema kuwa kamando wake mmoja, aliuwawa, na wengine watatu walijeruhiwa, katika shambulio dhidi ya makao makuu ya al-Qaeda nchini Yemen.
Ndege ya jeshi la Marekani iliyotumika katika shambulio hilo, ilielezewa kuwa ilitua kwa kishindo, na kujeruhi wanajeshi zaidi.
Jeshi linasema wapiganaji 14 waliuwawa, katika shambulio hilo lilofanywa alfajiri, katika jimbo la al-Baida.
Lakini watu wa huko, wanasema idadi ya waliouwawa ilikuwa kubwa zaidi, na wanasema raia kadha pia waliuwawa.
Wadadisi wanasema, shambulio hilo la kwanza la aina yake, tangu Rais Donald Trump kuapishwa, litaonekana kama ishara ya lengo lake la kutumia nguvu zaidi dhidi ya makundi ya wapiganaji wa Kiislamu.
0 maoni:
Post a Comment