MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Miili zaidi yatolewa eneo la maporomoko ya taka Ethiopia

Waokoaji wanatumia matingatinga na hata mikono yao kuondoa mawe na vifusi.Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaokoaji wanatumia matingatinga na hata mikono yao kuondoa mawe na vifusi.
Miili zaidi imetolewa kutoka kwa taka nyingi kwenye mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, ambapo karibu watu 50 waliuawa wakati wa maporomoko ya taka mwishoni mwa wiki.
Oparesheni kubwa ya uokoaji kwa sasa inaendelea huku mamlaka zikihofia kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka zaidi. Watu kadha bado hawajulikani waliko kufuatia mkasa huo.
Waokoaji wanatumia matingatinga na hata mikono yao kuondoa mawe na vifusi, wakati shughuli ya kuwatafuta manusura na wale waliokufa ikiendelea.
Waziri wa habari nchini humo Dr Negeri Lecho, anasema kuwa manusura wote watahamishiwa eneo lingine. Hadi sasa karibu familia 200 zimehamishwa.
Watu ambao walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo ya siku ya Jumamosi wametibiwa na kuruhusiwa kuenda nyumbani.
Bado haijulikani kilichosababisha kuporomoka kwa taka hiyo lakini waziri mkuu nchini Ethiopia, ametuma rambi rambi zake kwa familia zilizoathiriwa akisema uchunguzi wa mkasa huo utafanyika.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment