MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Nusu fainali Kombe la FA: Chelsea v Tottenham, Arsenal v Man City

Manchester City v Spurs 1981 FA Cup final replayHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDroo inatoa uwezekano wa marudio ya fainali ya 1981 kati ya Manchester City na Spurs, ambayo Spurs walishinda mechi ya marudiano
Mahasimu wa jiji la London Chelsea na Tottenham wamepangwa kukutana katika nusufainali Kombe la FA nchini Uingereza, Arsenal nao wakapangwa kukutana na Manchester City.
Arsenal watakuwa wanacheza nusu fainali Kombe la FA kwa mara ya 29
Nusu fainali zote mbili zitachezewa Wembley wikendi ya 22 na 23.
Chelsea walifuzu kwa kuwafunga Manchester United 1-0 Jumatatu.
Spurs walifika nusu fainali kwa kulaza Millwall 6-0 Jumapili.
Arsenal, ambao walishinda kombe hilo 2014 na 2015 waliwalemea Lincoln City 5-0 Jumamosi.
Manchester City ambao wanacheza nusu fainali kwa mara ya kwanza katika misimu minne, walifuzu kwa kulaza Middlesbrough 2-0 ugenini.

Kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment