MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Viongozi wa kijadi Australia wataka mkataba utakao watambua rasmi

 Jamii kutoka Arnhem
Viongiozi wa kijadi nchini Australia ambao wamekua wakikutana kujadili jinsi ya kutambuliwa na katiba ya nchi watatangaza azimio la pamoja Ijumaa.

Viongozi 250 wanakutana katika eneo la Uluru, ambapo ni chimbuko asili ya jamii za Aborigine tangu jadi.

Katiba ya Australia haitambui jamii asilia wala kuweka mikakati ya kuwalinda dhidi ya ubaguzi.
Kongamano la sasa linanuia kuwepo na azimio la pamoja kuhusu jamii asili za nchi hiyo.

Aidha azimio la Uluru linanuiwa kuwasilishwa kwa kura ya maoni ya kitaifa.

Jamii hii inaomba siyo tu kutambuliwa kisheria, lakini kuwa na uwakilishi maalum bungeni na nyathifa nyingine muhimu za kitaifa.

Pia wanataka kulipwa fidia kutokana na dhuluma za kihistoria.

kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment