MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Wauawa kwa kuwalinda wanawake Waislamu Marekani

 Polisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia kati
Polisi katika mji wa Portland nchini Marekani, wanasema wanaume wawili waliuawa, walipojaribu kumzuia mwanamume aliyewatukana kiubaguzi, wanawake wawili, walioonekana kuwa Waislamu.
Kisa hicho kilitokea kwenye treni jana.

Polisi wanasema mwanamume aliyekuwa akitukana, aliwageukia wanaume hao waliojaribu kuingilia kati, na kuwadunga visu na kuwauwa.

Abiria mwengine alijeruhiwa, kabla ya mshambuliaji kukamatwa.

Halmashauri ya uhusiano baina ya Marekani na Waislamu, imesema Rais Trump lazima atoe kauli kulaani chuki inayozidi dhidi ya Waislamu.

Imesema hali inazidi kuwa mbaya kwa sababu ya maneno ya rais na sera zake.

kutoka BBC swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment