Bada ya kuishi kwa muda wanandoa huanza kuonyesha dalili za kupungua kwa mapenzi yao waliyokuwa nayo awali. Iwapo Mwenyezimungu amewajaalia mtoto basi hapo mama anapata kisingizio cha kulea mtoto na hana muda tena wa kulea mume kama aliokuwa nao pale mwanzo, hapo utaona mume anaachiwa msichana wa kazi ndiyo amlee. Kitendo hiki cha kutomjali mume, humfanya mzee kukosa hamu hata ya kurudi nyumbani mapemaa.
Mume naye kama alikuwa anawahi kurudi nyumbani ndio mwanzo wa kuchelewa kurudi nyumbani na kila akirudi atasema amechoka, hana muda kabisa wa kukaa na mkewe kuongea juu ya maisha yao na jinsi ya kumlea mtoto wao. Kule kukumbatiana na mabusu ya awali pindi arudipo kazini ndo yamekwisha. Kila utakaye muuliza kati ya wanandoa hao atakwambia mwenzie ndiye aliyepunguza mapenzi kwake.
Nini cha kufanya ukiona mwenzio ameanza kupunguza bashasha alizokuwa nazo mwanzo?
Ukiona kuna upungufu wa mapenzi katika ndoa yako kuliko pale mwanzo, hutakiwi kwenda kwa mganga kutafuta ndumba, bali unachotakiwa kufanya ni kutumia Limbwata Spesho.
Kwanza, unapaswa kuzifahamu kwa undani tabia za mwenzio, ukishazijua tabia za mwenza wako itakusaidia kujua cha kufanya pindi ukiona mabadiliko ndani ya ndoa yako.
MWANAMKE:
Ukiwa kama mwanamke unapaswa kujua kuwa, wewe ndiye mlezi na muangalizi mkuu wa nyumba yako pamoja na vilivyomo ndani ya nyumba. Hapa ninamaanisha kuwa wewe ni mlezi mkuu wa mume na mali zake. Kwahiyo ukiona kuna mabadiliko ndani ya nyumba yako hakikisha mabadiliko hayo yanapatiwa ufumbuzi haraka.
Ukiona mumeo ameonyesha dalili za kupunguza mapenzi kwako, unachotakiwa kufanya ni kumlazimisha akupende bila ya mwenyewe kujijua huku ukiwa unafanya uchunguzi ili kujua kinachomsibu.
Kumlazimisha ninakozungumzia hapa si kwa kutumia nguvu wala matusi kama wanavyofanya wanawake wengi pindi waonapogundua kwamba kuna mabadiliko ndani ya mahusiano yao. !
0 maoni:
Post a Comment