Kwa mwenye mpenzi mpya
Kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati ukiwa na mpenzi wako
siku ya kwanza. Kati ya mambo hayo leo nitayaelezea mambo
ambayo unapaswa kuyaepuka au kuyazingatia siku hiyo.
(1) Chagua maswali ya kuuliza
Ili kutaka kuzifahamu mapema tabia za mpenzi mpya,
wapo wanaokimbilia kuuliza maswali hata yale yasiyostahili
kwa wakati huo.
“Hivi umeshawahi kuwa na wapenzi wangapi kabla yangu?
Unanilinganisha vipi mimi na wapenzi wako walionitangulia?
Kuna ambaye bado unamkumbuka kutokana na mapenzi
yake kwako na jinsi ulivyompenda?”
(2) Usimsifie wala kumponda mpenzi wa zamani
Wapo baadhi yetu wanaofikiri ukisifia mambo mazuri uliyokuwa
unafanyiwa na mpezni wako wa zamani basi huyu wa sasa ndio
atakupenda zaidi na kukufanyioa mambo mazuri zaidi. Si kweli.
“… alikuwa ananipenda sana na hata mimi nilikuwa nampenda,
yaani tulikuwa tunapenda. Alikuwa ananifanyia mambo mengi
mazuri.” Hutakiwi kuzungumza maneno haya mbele ya mpenzi
wako mpya, utaharibu uhusiano wako.
(3) Acha kujisifia
Kuna wanaopenda kujisifu na kujikweza ili waonekane bora
mbele ya wapenzi wao wapya. Kuna msemo wa wahenga waliosema
“kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.”
Ubora wa mtu unatokana na vitendo vyake si maneno.
Huna haja ya kuhubiri uzuri wako, wema wako au uwezo
wako wa “kucheza rumba” kwa mpenzi wako, yeye
mwenyewe atang’amua ubora wako baada ya kuwa nawe kwa muda.
Tabia ya mtu ni sawa na mapembe - haifichiki. Kama wewe ni
hodari wa “ndomboro” atakuona tu bila hata kujielezea.
Tulia aone mwenyewe.
(4) Fanya unaloweza
Usifanye kitu kwa kujilazimisha. Hakuna kuigiza kwenye
mapenzi, fanya kile unachoweza na usichoweza kiache.
Kuigiza katika mapenzi ni miongoni mwa sumu zinazoteketeza
upendo wa dhati.
Kwanini? Kwa sababu leo unaweza ukafanya jambo
fulani la kumfurahisha mpenzi wako, lakini umeigiza.
Umejilazimisha kufanya ingawa si fani yako. Umejitutumua
kulifanya ingawa lipo nje ya uwezo wako. Sasa balaa
litakuja wakati mpenzi wako atakapotaka urudie tena kufanya hivyo,
utashindwa kwa kuwa awali ulijilazimisha.
0 maoni:
Post a Comment