Kuwa mfano wa kuigwa
KARIBU msomaji wa safu hii ya kujuzana masuala
mbalimbali yahusuyo maisha katika familia zetu.
Katika safu hii, tunazungumza
kuhusu mapenzi
yanayoweza kuimarisha ndoa pamoja na malezi
bora ya familia.
Alhamisi ya leo tuna mada inayohusu mtu
anavyopaswa
kuishi katika jamii yake. Maisha ya ndani kwake, akiwa
na mkewe au
mumewe na watoto wake, na pia maisha
ya mitaani akiwa na jamii inayomzunguuka.
Kuna baadhi ya watu wanaishi kwa kutolewa
mifano mibaya
kutokana na vitendo vyao. Ndani ya nyumba zao hawaishi
kwa amani,
mitaani nako kila wanakopita wananyooshewa
vidole kwa vitendo vyao viovu.
Maisha ya watu wa aina hii ni maisha ya mikasa,
na mara zote
hudharaulika katika jamii. Wenye ndugu ambaye anasemwa
vibaya
katika jamii wakati mwingine wanajuta kuwa na ndugu
wa aina hiyo.
Hata mtoto mwenye mzazi ‘kituko’ huona aibu
mbele za
watoto wenziwe anaposikia vituko vya mzazi wake.
Unatakiwa utende matendo mazuri ili uwe kielelezo
cha
watu wengine kutenda mema. Kuwa mfano wa kuigwa
katika jamii yako kwa
kutenda matendo yatakayowapendeza
wengi. Usiwe mfano mbaya kwa kutenda matendo
yatakayo
wachukiza wengi.
0 maoni:
Post a Comment