Kuwa mfano wa kuigwa
KARIBU msomaji wa safu hii ya kujuzana masuala
mbalimbali yahusuyo maisha katika familia zetu. Katika safu hii, tunazungumza
kuhusu mapenzi yanayoweza kuimarisha ndoa pamoja na malezi bora ya familia.
Alhamisi ya leo tuna mada inayohusu mtu
anavyopaswa kuishi katika jamii yake. Maisha ya ndani kwake, akiwa na mkewe au
mumewe na watoto wake, na pia maisha ya mitaani akiwa na jamii inayomzunguuka.
Kuna baadhi ya watu wanaishi kwa kutolewa
mifano mibaya kutokana na vitendo vyao. Ndani ya nyumba zao hawaishi kwa amani,
mitaani nako kila wanakopita wananyooshewa vidole kwa vitendo vyao viovu.
Maisha ya watu wa aina hii ni maisha ya mikasa,
na mara zote hudharaulika katika jamii. Wenye ndugu ambaye anasemwa vibaya
katika jamii wakati mwingine wanajuta kuwa na ndugu wa aina hiyo.
Hata mtoto mwenye mzazi ‘kituko’ huona aibu
mbele za watoto wenziwe anaposikia vituko vya mzazi wake.
Unatakiwa utende matendo mazuri ili uwe kielelezo
cha watu wengine kutenda mema. Kuwa mfano wa kuigwa katika jamii yako kwa
kutenda matendo yatakayowapendeza wengi. Usiwe mfano mbaya kwa kutenda matendo
yatakayo wachukiza wengi.
0 maoni:
Post a Comment