VIONGOZI WA UAMSHO WAFIKISHWA KIZIMBANI
Viongozi saba wa kundi la kiislamu la Uamsho leo
wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya
Mwanakwerekwe huko kisiwani Zanzibar.
Mbele ya hakimu mkaazi wa mahakama hiyo,
viongozi hao wameshtakiwa kwa kosa la kusababisha
vurugu miezi miwili iliyopita.
Miongoni mwa masheikh waliopelekwa katika
mahakama ya Mwanakwerekwe iliyopo nje kidogo ya
mji wa Zanzibar ni pamoja na Sheikh Farid Hadi Suleiman,
Mselem Ali Mselem, Musa juma Issa , Suleiman Majisu
pamoja na Haji Sadifa ambaye ni mkuu wa usalama wa Uamsho.
Wakiwa kizimbani, viongozi hao wamesomewa shtaka lao la kusababisha vurugu visiwani humo tarehe 17 na 18 mwezi Agosti mwaka huu.

0 maoni:
Post a Comment