KWA
tamaduni za makabila mengi Tanzania titi la mwanamke limepewa thamani na
kuchukuliwa kama kiungo cha faragha. Halipaswi kuonyeshwa hadharani.
Titi
si kiungo kinachopaswa kuachwa wazi ili kila mwenye jicho aone. Titi lina
mahala pake pa kulionyesha. Na zaidi lina mtu wake anayepaswa kuliona na
kuligusa. Tena kwa wakati maalum.
Titi
lina sifa kubwa kuu mbili; kwanza kushibisha watoto na pili, kwa watu wengi
titi ni kiungo muhimu katika kunogesha mapenzi. Wengine titi wanaliita “chumvi”
ya mapenzi – chakula bila chumvi hakinogi. Titi hilo.
Ukimshika
mwanamke mkono, mguu, kichwa na hata jicho bila ridhaa yake hawezi kukushitaki.
Lakini mguse titi; akikushitaki umefungwa! Ujue titi si kiungo cha kawaida
katika mwili wa mwanake.
Lakini
siku hizi dada zetu wameacha utamaduni wa kulithamini titi. Imekuwa fasheni
kwao kuacha matiti wazi. Kwa mwanamke mwenye kujiheshimu hii ni kashfa kwake.
Sijui baada ya titi sehemu gani nyingine nyeti itafuata kuachwa wazi.
Titi
linalochukuliwa kama chumvi ya mapenzi halithaminiwi, kutakuwa na ajabu gani
tukiona chakula kinachonogeshwa na chumvi nacho kikiachwa wazi?
Wapo
dada zetu wanaochora matiti yao na kuyaanika hadharani. Bahati mbaya, wengi wao
wanafanya haya kwa kuiga na wala hawajui maana yake.
Titi
linachorwa na kuachwa wazi makusudi ili kila mwenye jicho aone. Aliyefikia
hatua ya kuonyesha titi wazi usimwamini, siku yoyote ataonyesha sehemu nyingine
nyeti.
Siku
hizi kuna sidiria zinazo nyanyua matiti na kuonekana kama jipu linalosubiri
kutumbuliwa. Wanaoacha wazi matiti wanafikiri wanaume wanaona wanawafagilia,
kumbe wengi wao wanawalaani na kuwadharau.
Wakati
wa utoto wangu ilikuwa vigumu kuona titi la msichana likiwa limeachwa wazi.
Lakini siku hizi haipiti siku bila kuona matiti ya wasichana yakiwa wazi.
Utapita
wapi usione msichana aliyepiga ‘jeki’ titi na kuliacha wazi? Ukiingia kwenye
ofisi nyingi utakutana na wasichana
waliopiga jeki matiti yao. Ukipanda daladala utawakuta wamesimamisha vifua na
ukiwa sehemu ya kupata kinywaji huko ndio kabisaa!
Kuna
baadhi ya wanaume wakiona tu titi wanasisimka hata kabla hawajaligusa na
wanawake wanalijua hilo. Shaka yangu ni kwamba, wanaume wakizoea kuona matiti
na wakaanza kupuuza dada zetu wataamua kutuonyesha sehemu gani nyingine nyeti?
Titi
ni miongoni mwa viungo adhimu kwenye mapenzi. Baadhi ya wanaume wanapata
msisimko mkubwa wanapogusa titi la mwanamke, na hata baadhi ya wanawake
wanapata msisimko wa ajabu wanapoguswa matiti na mwanaume.
Titi lina mvuto wake bwana; kuna titi la dodo, bolibo na hata
papai. Lipo pia titi la boga. Kwa baadhi
wa wanawake na wanaume wanatumia titi kufikishana kileleni. Titi hilo.
Hata
wale wanawake wenye kunyonyesha hadharani hawatakiwi kuliacha wazi titi.
Unaweza kumwona mwanamke ananyonyesha mtoto ndani ya daladala na kuliachia titi
kila aliyomo ndani ya daladala alione.
Sisemi
watoto wakitaka kunyonya kwenye daladala wasinyonyeshwe, la hasha. Ninachosema
kuwepo na ustaarabu wa kulificha titi hata wakati wa kunyonyesha. Mbona
wanawake wengine wanaweza kunyonyesha mbele za watu na titi lake lisionekane?
Kuna
sehemu zake za kuacha titi wazi na kuna watu wake wanaopaswa kuonyeshwa, kuligusa
na hata kulichezea. Titi lipewe thamani yake. Sijui baada ya titi tunaonyeshwa
nini. Tusubiri.


0 maoni:
Post a Comment