Wapigani wa waasi nchini
jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wametishia kuendeleza mapigano hadi mji mkuu
wa nchi hiyo Kinshasa, siku chache tu baada ya kuuteka mji wa Goma.
Msemaji wa kundi hilo la waasi wa M23 rLt Col
Vianney Kazarama amewaambia watu waliokuwa wamekusanyika mjini Goma kuwa wako
tayari kukomba taifa hilo.Awali Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linalolaani kutekwa kwa mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na waasi wa M23.
Azimio hilo pia linamtaka katibu mkuu wa Umoja huo kuripoti kuhusu madai ya uungwaji mkono wa mataifa ya kigeni kwa makundi ya uasi yaliyoanza harakati zao nchini Congo miezi minane iliyopita.

0 maoni:
Post a Comment