CAF imetangaza orodha fupi ya
majina ya wachezaji ambao wamo katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa tuzo ya
mchezaji bora zaidi barani Afrika.
Mshindi wa mwaka jana, Yaya Toure, anaongoza
katika orodha hiyo yenye majina ya wachezaji 10, waliochaguliwa kutoka orodha
ndefu ya wachezaji 34. Mchezaji huyo kutoka Ivory Coast, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Manchester City, ni kati ya wachezaji wanne wanaozichezea timu za Uingereza ambao huenda wakapata tuzo hiyo ya mwaka 2012. Wachezaji hao ni John Obi Mikel wa Chelsea, Alexandre Song, Didier Drogba,
Chris Katongo wa Zambia, na mchezaji wa Morocco , Younes Belhanda, na wengine kibao

0 maoni:
Post a Comment