Timu ya taifa ya soka ya Afrika
Kusini, imetangaza kikosi chake ambacho kitapambana na Zambia katika mechi ya
kirafiki.
Afrika Kusini imeamua kuwaalika wachezaji
wake nchini Ubelgiji, Darren Keet na Anele Ngcongca katika mechi hiyo dhidi ya
mabingwa wa Afrika, Zambai.Pambano hilo litachezwa tarehe 14 mwezi Novemba.
Keet ni kati ya walinda lango wawili wa timu hiyo, naye mlinzi wa timu ya Genk, Ngcongca, amechaguliwa kwa mara ya kwanza na kocha wa timu ya taifa, Gordon Igesund.
Kufuatia Steven Pienaar kustaafu kutoka mechi za kimataifa, mlinzi wa zamani wa Tottenham ya Uingereza, Bongani Khumalo, sasa ataiongoza timu hiyo kama nahodha.

0 maoni:
Post a Comment