Baada ya kampeni za miezi kadhaa ,
vituo vya kupiga kura vinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni katika uchaguzi
wenye ushindani mkali na ambao ulikuwa na kempeini zenye kugharimu pesa nyingi
zaidi kuwahi tumika katika historia za uchaguzi Marekani
.
Rais Obama alitoa wito wake wa
mwisho kwa wapiga kura katika mkutano wa kisiasa uliofanyika katika jimbo la
Iowa hapo jana.
Ushindani katika uchaguzi huu ni
mkali sana na mpinzani wa rais Obama wa chama cha Republican Mitt Romney
amekuwa akiyazuru mara kwa mara majimbo mawili makuu Ohio na Pennsylvania.
Kura ya mwisho ya kutafuta maoni
iliashiria kuwa rais Obama anaongoza katika majimbo mengi ambayo wagombea wote
wana nafasi.
Lakini kura hiyo inaashiria pia
huenda idadi ya watu watakao jitokeza kupiga kura ikawa kubwa miongoni mwa
wafuasi wa Romney
Kura za kwanza zilipigwa katika eneo
la Dixville Notch katika jimbo la New Hampshire ambapo wagombea wote walitoka
sare.

0 maoni:
Post a Comment