Chelsea wiki hii ina kibarua
kigumu, mbali tu na kuangazia mechi dhidi ya Shakhtar Donetsk na Liverpool.
Wachezaji, makocha na pia wafanyakazi wa
klabu hiyo ya London, huenda wakawapokea maafisa kutoka chama cha soka cha FA, na
vilevile wale wa idara ya polisi ya Metropolitan. Wote watakuwa na nia ya kuthibitisha yaliyotamkwa na mwamuzi Mark Clattenburg, au kutosemwa, wakati timu ya Chelsea ikiwa uwanja wa nyumbani, na maarufu kwa jina The Blues, iliposhindwa na Manchester United, katika uwanja wa Stamford Bridge, tarehe 28 Oktoba.
Mazungumzo kati ya wahusika wote yataamua kama Clattenburg atashtakiwa kwa kutumia lugha isiyofaa, dhidi ya mchezaji wa kimataifa wa Nigeria, Jon Obi Mikel, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Chelsea.

0 maoni:
Post a Comment