Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini
Marekani yameanza kutolewa kutoka maeneo mbali mbali ya nchi.
Rais Barack Obama ameshinda katika
majimbo ambayo yalikuwa muhimu sana kubaini mshindi wa uchaguzi huu ambayo ni Michigan
na Pennsylvania, pamoja na mengine ambayo alishinda katika uchaguzi wa mwaka
2008.
Mwenzake wa Republican Mitt Romney ameshinda
katika majimbo mengine muhimu pia ya Republican pamoja na kushinda Indiana
ambalo lilimuunga mkono Obama mwaka 2008.
Mamilioni ya watu walijitokeza
kupiga kura siku ya Jumanne. Mshindi huenda akajulikana baada ya masaa kadhaa
kuanzia sasa hususan huku matokeo katika majimbo mengine muhimu yakitolewa.
Kura za maoni kabla ya kufanyika
uchaguzi huu zilionyesha kinyang'anyiro kitakuwa kikali ingawa zilimpa ushindi
wa kura chache tu Rais Obama katika majimbo kadhaa muhimu.
Vituo vya kupigia kura vilianza
kufungwa mapema katika maeneo ya Mashariki mwa nchi , huku majimbo ya Virginia
na Ohio nayo yakifunga mapema.
Kwa sasa kura za Electoral College
zinaonyesha Obama yuko nyuma ya Romney kwa kura sita


0 maoni:
Post a Comment