Serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuichukulia hatua Rwanda,
kwa madai ya kusaidia waasi nchini Congo badala ya kumfuatilia mtu mmoja kama
vile kanali Sultani Makenga.
Waziri wa habari wa serikali ya Congo amesema
hayo siku moja baada ya Umoja wa Mataifa na Marekani kutangaza vikwazo dhidi ya
kiongozi wa waasi wa M23, Jenerali Makenga, vikiwemo vya usafiri na kukamata
mali yake.Serikali ya Marekani pia imewazua Wamarekani kujihusisha kwa namna yoyote na Sultan Makenga, ambaye alikuwa afisa wa ngazi ya cheo cha Jenerali katika jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

0 maoni:
Post a Comment