Timu ya soka ya Tanzania taifa staz imewatoa
kimasomaso mashabiki wake
Baada ya kuifunga timu ya taifa ya Kenya , Harambe
staz kwa mabao 1-0 katika
Mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa leo
katika kiwanja cha CCM KIRUMBA
Mjini mwanza ,
Bao pekee la stars lilipachikwa kimiayani kwa kichwa
na beki kisiki wa stars Agrey morris
Dakika ya 7 ya mchezo akiunganisha pasi ya salum
abubakar[sure boy] ambaye naye alipokea
Mpira wa kona uliyopigwa na Amir Maftaha .
Timu ya Kenya ikiongozwa na nahodha wake dennis
oriech, walijaribu mara kadhaa kutaka
Kusawazisha bao hilo, lakini ngome ya stars ikiwa
chini ya mlinda mlango na nahodha wake ,
juma kaseja , ilikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa
Harambee Stars


0 maoni:
Post a Comment