Patrick Viera amesema anataka
kocha wa Manchester City, Roberto Mancini kusalia katika klabu hiyo, ili
kuiongoza kushinda medali zaidi.
Mancini alisaini mkataba mpya na klabu hiyo
mwezi Julai mwaka huu, baada ya kuiongoza kushinda kombe la ligi kuu ya Premier
msimu uliopita, lakini katika siku za hivi karibuni kumekuwa na fununu kuhusu
hatma ya kocha huyo.Vieira, ambaye ni afisa mkuu anayehusika na masuala ya uendelevu wa soka katika klabu hiyo, amesema Mancini, alisaini mkataba wa miaka mitano na hiyo ni ishara kuwa ana imani na klabu ya Manchester City.

0 maoni:
Post a Comment