Shirika la reli nchini Kenya
limezindua treni mpya ambayo ina mwendo wa kasi ili kutoa huduma kwa wakaazi wa
viungani mwa mji wa Nairobi.
Ni treni ya kwanza ya aina yake
kuzinduliwa tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka 1963.
Treni hiyo itatoa usafiri kati ya
mji mkuu na mtaa wa Syokimau na viunga vyake, viungani mwa Nairobi ambako
serikali imejenga kituo cha treni ambacho ni cha kwanza kukamilishwa chini ya
mradi wa ukarabati wa mfumo wa reli ambao unafanyika kwa mara ya kwanza kwa
miaka 80.

0 maoni:
Post a Comment