Juhudi za uokozi katika jengo la
ghorofa lililoporomoka wiki jana nchini Ghana zimesitishwa.
Kwa mujibu wa maafisa waliokuwa
wanasimamia shughuli hiyo, mjini Accra, idadi ya watu waliofariki imefika 14,
wala sio kumi na nane kama ilivyoripotiwa hapo awali huku watu wnegine 67
wakinusurika.
Ujenzi mbovu umelaumiwa kwa kuanguka
kwa jengo hilo lenye maduka na amblo lilifungua rasmi mapema mwaka huu.
Mmiliki wa jengo hilo, pamoja na
afisaa anayesimamia ubora wa majengo, wamezuiliwa.
Rais John Dramani Mahama, alisema
kuwa wale waliohusika na kupuuza usalama na ubora wa jengo hilo lazima
watachukuliwa hatua kali.

0 maoni:
Post a Comment