Polisi nchini Uganda wamewazuia
wanaharakati wa kupinga ufisadi kufanya maandano katika barabara za mji mkuu wa
nchi hiyo, Kampala.
Karibu wanaharakati 300 waliokuwa wamevalia
nguo nyeusi walilazimika kukatiza maandamano yao baada ya polisi waliojihami kwa
silaha kuziba barabara zote.maandamano hayo yamefanyika kufuatia ufichuzi katika vyombo vya habari kuhusu visa kadhaa vya ufisadi ikiwemo madia kwamba zaidi ya dola milioni 15 za misaada ya kigeni zimeishia mifukoni mwa wakuu fulani serikalini.

0 maoni:
Post a Comment