MKUTANO WAMALIZIKA KUJADILI HATMA YA
DRC
Viongozi wa Afrika wamewasihi
wapiganaji mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuacha mashambulio.
Mwisho wa mkutano wao mjini Kampala,
Uganda, viongozi hao wamewataka wapiganaji wa kundi la M23 waondoke kutoka mji
wa Goma waliouteka hivi karibuni.
Viongozi hao piya walimsihi Rais wa
Congo, Joseph Kabila, kushughulikia malalamiko ya wapiganaji.
Viongozi wane walihudhuria mkutano
huo - Rais Paul Kagame wa Rwanda hajakuwepo.
Rwanda inashutumiwa kuwa inawasaidia
wapiganaji wa M23 - shutuma inazokanusha.

0 maoni:
Post a Comment